Pendo
Adolph Manyama (29) na watoto wake wawili, wakazi wa Kola katika
Manispaa ya Morogoro, wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuungua na
moto uliyosababishwa na kulipuka kwa jiko la gesi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Wilbrod Mutafungwa, alisema jana kuwa
tukio hilo lilitokea Desemba 26, mwaka jana, saa 10:30 jioni , maeneo ya
Kola, Manispaa ya Morogoro.
Mutafungwa
alisema siku hiyo mtoto wa mama huyo aliyejulikana kwa jina la Angela
Baltazar (4) alifungua mtungi wa gesi na kusababisha gesi kujaa ndani ya
nyumba hiyo.
“Wakati
mtoto akifungua mtungu huo, mama yake ambaye alikuwa Mwalimu wa shule
ya Msingi Forest, bila kujua aliingia ndani na jiko la mkaa na
kusababisha moto kulipuka na kumuunguza yeye na watoto wake wawili,
jambo lilosababisha vifo vyao,” alisema.
Aidha,
Kamanda Mutafungwa aliwataka wananchi kuwa waangalifu wakati wote
wanapokuwa wanatumia vyombo hivyo vya majumbani, ili kuepusha ajali
mbalimbali za moto kutokea.
Mmoja
wa jamaa wa karibu na familia hiyo, alielezea tukio hilo lilitokea
Jumatano iliyopita wakati mume wa mama huyo, Baltazar Kineneko (37)
akiwa mkoani Arusha kikazi.
“Ilikuwa
majira ya usiku mama akiwa anapika kibarazani kwenye jiko la mkaa mtoto
wa miaka minne aliingia ndani na kuchezea jiko la gesi, gesi ikawa
inavuja.
Mtoto alipofungua mlango kutoka nje mvutano wa gesi na mkaa ulisababisha mtungi wa gesi kulipuka hadi juu na kutoboa gypsum.
“Mama aliingia ndani kumuokoa mtoto, lakini alitoka akiwa anaungua mwili mzima. Mtoto wake mwingine wa miaka sita
aliyekuwa
nje anacheza alipoona mamaye anatoka ndani na mdogo wake huku wakiwa
wanaungua moto alikimbia kumkumbatia mama yake naye akaanza kuungua,”
alieleza jamaa huyo.
Ndugu
huyo alisema mama na mtoto mdogo walikufa papo hapo, mtoto mkubwa
alisafirishwa kwa ndege kwenda Nairobi nchini Kenya kwa matibabu baada
ya hali yake kuonekana mbaya.
Hata
hivyo, jamaa huyo alisema baba wa mwanamke aliposikia kuwa mwanaye na
mjukuu wamekufa alipata mshtuko naye akafa hapo hapo, alizikwa jana
mkoani Morogoro.
“Baba
wa mtoto yaani mume wake yule mama katoka leo (jana) Nairobi, ili kesho
(leo) amzike mke na mwanaye kisha arudi Nairobi kumuuguza mwanaye
aliyebaki, lakini usiku wake akiwa safarini alipigiwa simu kuwa mtoto
aliyemwacha
Nairobi naye kafariki,” alieleza mtu huyo.
Alisema baba huyo yupo katika wakati mgumu hiyo anawaomba watanzania wamuombee, ili aweze kulikabili jambo hilo.
Mpekuzi.
Comments