Amesema kuna baadhi ya watu
wamekuwa wakiwatumia vibaya wasomi kwa kuwadanganya kutokana na
maendeleo yaliopo nchini baada ya Mapinduzi.
Akizungumza wakati
akifungua kongamano la chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA, la
kuadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukumbi wa Suza
majestic, Mhe Riziki amesema kuna maendeleo mbali mbali yamepatikana ikiwemo Elimu bure ambapo awali hayakuwepo.
Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais Dk. Ali Mohamed
Shein, itaendelea kusimamia ilani ya chama cha Mapinduzi na itahakikisha
watu wote wanapata huduma za msingi ikiwemo Elimu bure, afya, maji safi
na salama pamoja na kuimarisha huduma za miundombinu mbali mbali
nchini.
Hivyo amewataka wasomi hao kuthamini juhudi za Serikali yao pamoja na matunda ya Mapinduzi na kujivunia Uhuru wao na kutokubali kutawaliwa katika nyanja mbali mbali.
Nae Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar Suza, SUZASO ndugu Khamis Kea Juma amesema miongoni mwa waathirika wa Mapinduzi ni wasomi, hivyo wamejiandaa kuinesha maendeleo ya Elimu kutoka kipindi cha ukoloni, tulipo sasa na muelekeo wa baadae.
Akiwasilisha maada katika kongamano hilo,mhadhiri msaidizi SUZA, Mr khalfan Salim Suleiman amesema wizara ya Elimu imepiga hatua katika suala zima la utoaji wa Elimu bora, hivyo ameomba kuboreshwa katika kuwekwa kituo cha kumbumbuku ambacho kitaweza kutoa taarifa mbalimbali, kituo cha utafiti wa Elimu ili wasomi hao wasiweze kudanganywa.
Pia amekiomba chama cha Mapinduzi kuandaa Sera ya kuendeleza Elimu kwa wanachama wa chama cha Mapinduzi ili wasiweze kudanganywa wanachama wachanga wa chama hicho.

Comments