Mkuu wa Kitengo cha Takwimu za Bei Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa
Serikali, Khamis Abdul-rahman Msham, alisema, mfumko wa bei za vyakula
na vinywaji visivyo na kilevi ulipungua kwa asilimia 2.2 ikilingwanishwa
na asilimia 3.4.
Alisema, faharisi za bei ziliongezeka na kufikia 108 mwezi Disemba ikilinganishwa na 105.1 zilizorikodiwa Disemba 2017.
Alisema, kiwango cha mwaka cha mfumko wa vyakula ulishuka hadi
asilimia 2.3 mwezi Disemba ikilinganishwa na asilimia 3.5 kwa mwaka
ulioishia Novemba 2018.
Faharisi za bei za vyakula ziliongezeka hadi 106.7 mwezi Disemba kutoka 104.3 kwa mwezi Disemba 2017.
Mkuu huyo, alisema, kwa upande wa bidhaa zisizokuwa za vyakula,zilishuka hadi asilimia 4.3 ikilinganishwa na 5.2.
Alizitaja bidhaa zilizochangia kushuka kwa kiwango zilikuwa mchele
wa Mbeya (6.5%), sembe (19.5%), unga wa ngano (0.4%), ndizi za mtwike
(21.6%), ndizi za mkono mmoja (10.3%) na sukari (4.9%).
Kwa upande wa mfumko wa mwezi, uliongezeka kwa asilimia 0.6 mwezi
Disemba ikilinganishwa na asilimia ghasi 0.3 kwa mwezi Novemba 2018.
Alisema, kiwango cha mfumko wa bei cha vyakula na vinywaji visivyo na
vilevi kiliongezeka hadi asilimia 3.4 mnamo Novemba 2018 kutoka
asilimia 2.6 mwezi Oktoba 2018.
Mfumko wa vyakula na vinywaji visivyo na vilevi uliongezeka hadi 1.6
ikilinganishwa na asilimia ghasi 0.5 ambapo ongezeko hilo la mwezi
kulichangiwa na kuongezeka kwa bidhaa kama mchele wa Mbeya (0.8%) na
samaki (11.8%).
Alizitaja bidhaa nyengine ni mafuta ya taa (4.5%), petroli (1.7) na diseli (2.0%).
Mkuu wa Takwimu za Kiuchumi Ofisi ya Mtakwimu Mkuu, Abdulrauf
Ramadhan Abeid, alisema, bado mfumko unaendelea kubakia chini ya
tarakimu moja katika nchi za Afrika Mashariki na hivyo kwenda vizuri
kiuchumi.
Zanzibarleo.
Comments