Watu
wawili wamenusurika kifo baada ya lori aina ya scania walilokuwa
wakisafiria kutoka Dodoma kwenda Iringa kuigonga treni ya mizigo katika
makutano ya reli na barabara eneo la hazina jijini Dodoma.
Tukio
hilo lilitokea jana mchana mara baada ya lori hilo lenye namba za
usajili T463 ADW likiwa na tela lenye usajili T483 BLP kuiigonga treni
hiyo iliyokuwa ikitoka jijini Dar es salaam kuelekea mikoa ya kanda ya
ziwa.
Baadhi
ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa ajali hiyo imechangiwa na mvua
zilizokuwa zikinyesha na kumfanya dereva wa lori kutoona kizuizi cha
treni mbele yake.
Mmoja
wa mashuhuda hao Ramadhani Rashid Mkazi wa Majengo amesema kuwa ajali
hiyo ilichangiwa na dereva wa lori kutaka kukatiza kwa mwendo mkali
lakini alikuwa kacheleWa hali iliyosababisha kugongwa na treni hiyo ya
mizigo.
“Dereva
wa lori alikuwa katika mwendo mkali wakati akikatiza kivuko cha reli
hivyo alishindwa kusimama na treni likawa limekaribia na kumgonga
tumetoa watu wawili wakiwa wamejeruhiwa vibaya mwingine mmoja utumbo
ukiwa nje”alisema
Kaimu
kamanda wa polisi mkoani Dodoma ACP William Mkonda, amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo ni uzembe wa dereva wa lori
ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi na majeruhi wamelazwa katika
hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma
Comments