Alisema vijana wake wapo vizuri na wana ari kubwa sana ya mechi hiyo,
kwani wamewajenga kisaikolojia ili kuhakikisha wanashinda mchezo huo na
kutinga hatua ya fainali.
Alisema kuwa wanatambua kuwa mchezo huo utakuwa mgumu, lakini tayari
wameisoma timu ya Azam na wanajua jinsi ya kuwakabili baada ya kubaini
mapungufu yao.
‘’Najua ni mchezo mgumu, ni mabingwa watetezi watahakikisha wanacheza
ili kushinda na kujiweka nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao, lakini na
sisi tumejipang ili kulitwaa taji hilo’’alisema.
Alisema mashirikiano ambayo yapo baina ya viongozi na wachezaji kwa
kiasi kikubwa yanazidisha hamasa ya kuhakikisha mchezo huo wanaibuka na
ushindi.
Kwa upande wake kocha msaidizi wa timu ya Malindi Ahmed Salehe
Machupa,alisema mikakati yao ni kufanya vyema katika mechi yao na timu
ya Simba ili kuhakikisha wanafikia malengo.
Alisema kuwa timu ya Simba ni timu kubwa lakini kwao wanaichulia ya
kawaida, hivyo hana wasiwasi na watahakikisha wanacheza ka nguvu zote
ili kushinda na kuingia fainali.
“Timu ya Simba ni kama timu nyengine na hakuna ambacho tunakiogopa kwao’’alisema.
Nusu hizo zitachezwa leo katika uwanja wa Amaan, ambapo majira ya saa
10:15 jioni Azam itakipiga na KMKM na saa 2:15 usiku Simba itakuwa
uso kwa uso na Malindi.
Comments