kwa tatizo la kuingiliwa na maji taka katika eneo
hospital na skuli ya Bwejuu Dongwe imekuwa ni changamoto kwa wakaazi wa
kijiji hicho.
Akizungumza na muandishi wa
habari hizi Chum Haji Ali mwenye umri wa miaka 58 amesema baada
kuhamasika kupitia Mradi wa PAZA wameunda kamati yakufuatilia tatizo la maji
katika ofisi ya Halmashauri ya wilaya kusini lakini limeshindikana na maafisa
wa maji katika ofisi hiyo wamesema suali la maji watalifuatilia katika ofisi ya
mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) lakini hadi sasa hakuna dalili za upatikanaji
wa maji katika eneo hilo.
Akizungumzia kuhusiana na
huduma za Afya katika kijijini hapo amesema kwa sasa zimeboresha na kwa upande
wa wazazi wamepewa maelekezo endapo watakaopokua tayari kujifungua waelekee
spitali ya Jambiani.
Kwa upande wa elimu amesema
wanaushukuru mradi wa PAZA kwa kuwafanyia marekebisho Banda moja la Skuli na
kuutaka mradi huo kuendelea
kumehamasisha watu kujua utaratibu wa kwenda ofisi ya Halmashauri
kufuatilia changamoto zinazowakabili.
Nae Afisa Maji Wilaya ya
Kusini Bw Hafidhi Hassan Mwinyi amesema Baadhi ya shehia ya Bwejuu maji
yanapatika lakini eneo la Bwejuu Dongwe kuna mwinuko wa ardhi ndio imepelekea
waakaazi wa eneo hilo kukosa maji safi na salama .
Hata hivyo ameeleza kwamba
hatua za ufumbuzi zinaendelea kushughulikwa hivyo amewaomba wananchi waendelee
kustahamili huduma ya maji safi na salama itapatikana .
Kutokana na baadhi ya
changamoto walizonazo wanakiji cha Bwejuu Dongwe hazijatatuliwa wamekiomba Chama Cha Waandishi wa Habari
Zanzibar (TAMWA-ZANZIBAR) kuendeleza maradi wa kukuza Uwajibikaji Zanzibar
(PAZA) kutokana na tatizo la maji safi na salama bado halijatatuliwa katika
shehia hiyo.
Na RAHMA MOH’D
Comments