Hatimaye utawala wa Marekani imemuachulia huru
bila kumfugulia mashtaka mtangazaji wa Press TV, Bi. Marzieh Hashemi baada ya
kumshikilia kizuizini kinyume cha sheria kwa muda wa siku 11.
Katika taarifa,
familia yake imesema Bi. Hashemi ameachiliwa huru mjini Washington DC
pasi na kufunguliwa mashtaka.
Jana Jumatano
alifika mbele ya Jopo la Mahakama lenye wanachama 23 na duru zinasema
aliachiliwa baada ya ushahidi wake kusikilizwa.
Taarifa ya familia yake imesema.
Bi Marzieh Hashemi
ametoa wito kwa watu wote duniani kuendeleza maandamano ya kupinga mfumo wa
sheria nchini Marekani.
Taarifa hiyo
imesema, 'kama ambavyo Wamarekani wanafahamu watu weusi wanakandamizwa nchini
humo, hivi sasa Wamarekani pia wanapaswa kuzungumza kuhusu namna Polisi ya
Upelelezi Marekani, FBI, inavyowakandamiza Waislamu.
" Taarifa hiyo
imesema Bi. Marzieh Hashemi atashiriki katika maandamano makubwa mjini
Washington DC siku ya Ijumaa na kuongeza kuwa, kadhia si ya Bi. Hashemi pekee,
bali inahusu kila mtu, Mwislamu na asiyekuwa Mwislamu anaweza kushikiliwa
korokorini Marekani bila kufahamishwa makosa yake.
Wakati huo huo Mkuu
wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran, IRIB, Dkt. Peyman Jebeli amesema Marekani imelazimika kumuachilia huru
Bi. Hashemu kutokana na mashinikizo ya fikra za umma.
Amesema kuna haja ya
kuzidi kushadidisha harakati za kuamsha fikra za umma nchini Marekani ili nchi
hiyo iwaachilie wale wote inaowashikilia kinyume cha sheria.
Aidha amesema kuachiliwa
huru Bi. Hashemi ni mafanikio makubwa kwa vyombo huru vya habari hasa
televisheni za Press TV na Al Alam.
Bi. Marzieh Hashemi, Mmarekani mwenye asili ya
Kiafrika, anayefanya kazi na Televisehni ya Press TV ya hapa Tehran ambaye
alikuwa akiitwa Melanie Franklin kabla ya kusilimu, alitiwa nguvuni Jumapili ya
tarehe 13 Januari katika Uwanja wa Ndege wa St. Louis, Missouri na kupelekwa
mjini Washington DC alikoshikiliwa kwa muda wa siku 11.
Akiwa korokoroni, Marzieh Hashemi alivuliwa hijabu
yake na kulazimishwa kula nyama ya nguruwe ambayo ni haramu kwa Waislamu,
kitendo ambacho ni ukiukwaji wa wazi wa matukufu na thamani za Kiislamu.
Aidha mbali na
kumnyima chakula halali, wakuu wa Marekani pia walikataa kumpa Bi. Hashemi nguo
zinazofaa katika msimu huu wa baridi kali nchini humo.
parstoday.
Comments