Alisema sekta ya michezo ina ushawishi mkubwa miongoni mwa Jamii na inaweza kutumika vyema katika mapambano hayo, na kuleta mafanikio makubwa katika jitihada za kukabiliana na kadhia hiyo.
Balozi Seif Ali Iddi ametoa kumbusho hilo wakati akikabidhi zawadi
kwa timu ya soka ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) iliyotwaa ubingwa wa
Ligi Kuu ya Zanzibar kwa Mwaka 2018/2019 na mshindi wa Pili timu ya
Kikosi cha Zimamoto na Uokozi hafla iliyofanyika ofisini kwake Vuga
Mjini Zanzibar.
Vifaa hivyo vilivyoambatana na shilingi milioni 2,000,000/- kwa JKU
na milioni 1,000,000/- kwa Zimamoto, vilivyotolewa na mdau wa michezo
Mohamedraza Hassanaali ni pamoja na seti za jezi, viatu, mipira, pea 40
za viatu kwa timu ya wanawake ya mpira wa Pete ya JKU pamoja na seti ya
jezi kwa timu zote za Vikosi vya SMZ.
Comments