Watu wawili wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya Totota Hiace walilokuwa wamepanda kuacha njia na kupinduka.
Kamanda
wa Polisi mkoani Rukwa, George Kyando, alisema kuwa tukio hilo
lilitokea juzi majira ya alasiri. Aliwataja watu waliofariki katika
ajali hiyo ni Augenia Masumbuko (53) mkazi wa Isale, na Nestory Kayumba
mkazi wa Kalambo.
Kamanda
huyo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva aliyekuwa akiendesha
gari lenye namba za usajili T 795 CVA aina ya Toyota Hiace kushindwa
kulimudu katika mteremko, hivyo kuacha njia na kupinduka.
Katika
ajali hiyo watu wawili pia walijeruhiwa ambao ni Akoba Kung'ombe (40)
mkazi wa Bangwe na mwingine ambaye hajafahamika ambaye ni mwanaume
mwenye umri kati ya miaka 25-30.
Kamanda
Kyando alisema miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika kituo cha afya
Namanyere, na majeruhi wamelazwa katika Zahanati ya Myula kwa ajili ya
matibabu.
Kwa
mujibu wa Kamanda Kyando, dereva wa gari hilo alikimbia baada ya ajali
hiyo na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka ili afikishwe
mahakamani.
Aliwaasa
madereva mkoani humo kwa makini wawapo barabarani na kufuata sheria za
usalama barabarani, ili kuepuka vifo na majeruhi kutokana na ajali
zinazoweza kuepukika.
Comments