Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeiagiza Mamlaka ya Mawasiliano
nchini (TCRA) kusajili mafundi wanaotoa huduma za matengenezo ya simu za
mkononi kwa mujibu wa sheria zilizopo na kuhakikisha huduma wanaozotoa
kwa wananchi zina viwango stahiki.
Agizo
hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Sekta ya Mawasiliano
Dk Jim Yonaz jana Jumatano Disemba 5, alipokuwa akiwatunuku vyeti vya
kuhitimu mafunzo ya miezi mitano kwa mafundi simu 68 yaliyotolewa katika
Chuo cha Sayansi na Teknolojia (DIT).
Dk
Yonaz amewataka mafundi simu hao kutumia elimu waliyoipata katika
mafunzo hayo wakaitumie kwa kuwahudumia wananchi kwa uadilifu mkubwa na
kuwa mfano kwa mafundi wa aina hiyo hapa nchini.
“Kuanzisha
mafunzo haya ya kurasimisha ufundi wa simu za mkononi kutawasaidia
mafundi kufanya kazi kwa weledi na ufahamu lakini pia itaisaidia TCRA
kutoa leseni kwa mafundi ambao kiwango chao kinafahamika.
“Yamekuja
kwa wakati muafaka na naomba yaendelee kusimamiwa vyema ili mafundi
simu za mikononi nchini kote waweze kupata elimu hii, ” amesema Dk
Yonaz.
Aidha
Dk Yonaz ametoa rai kwa wadau wa Mawasiliano nchini kubuni mipango
endelevu ya kushirikiana kuchangia katika kufanikisha mafunzo hayo.
Mpekuzi.
Comments