Watu
168 mpaka sasa wameripotiwa kupoteza maisha huku 750 wakijeruhiwa
vibaya nchini Indonesia baada ya Tsunami kuikumba nchi hiyo siku ya jana
usiku.
Mamlaka
nchini humo zinasema Tsunami hiyo imetokea katika fukwe za visiwa vya
Java na imesababishwa na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mlipuko
wa volkano.
Msemaji
wa Taasisi inayoshughulika na kuzuia majanga nchini humo, Sutopo Purwo
Nugroho amesema mpaka sasa watu 30 hawajulikani walipo, huku nyumba 558,
migahawa 60 ikibomolewa na Tsunami.
Nugroho amesema tukio hilo ni la kushtukiza, kwani hakukuwa na taarifa wala tahadhari yoyote ile iliyotolewa kwa wananchi.
Usiku
wa Jumamosi siku ya tukio, Bendi ya muziki maarufu nchini humo ya Band
Seventeen, ikiongozwa na msanii wa muziki, Riefian Fajarsyah nayo
ilipatwa na kazia baada ya jukwaa lao kufunikwa na maji.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Riefian Fajarsyah amethibitisha kuwa watu wanne kutoka kwenye bendi yake wamefariki dunia.
Mwezi
kama huu mwaka 2004, tsunami kama hiyo ilitokea katika bahari ya Hindi
kufuatia tetemeko la ardhi, iliua zaidi ya watu 226,000 katika nchi 13
ikiwa 120,000 walikufa nchini Indonesia.
Comments