
Akiuliza swali la Msingi katika Mkutano wa Baraza la Wawakilishi
Mwakilishi wa Jimbo la Paje Jaku Hashim Ayoub alietaka kujua Serikali
ina Mpango gani wa Kuingiza mafuta kwa bei nafuu.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo Juma Makungu Juma amesema ni kweli bei za
mafuta zinashuka na kupanda kutoka na mabadiliko ya bei kutoka katika
soko la dunia.
Amesema mafuta yanayotumika Zanzibar huagizwa na makampuni manne
ambayo kabla ya kufikishwa Zanzibar Mafuta hayo huhifadhiwa katika
Bohari ya Dar es salam na Bandari ya Mombasa ambapo makampuni hayo
hulazimika kulipa kodi na kupelekea bei ya mafuta kupanda.
Aidha amesema tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi baada ya kujengwa
miundombinu ya mafuta ikiwemo Bandari na Matangi itakayowezesha meli
kubwa za mafuta kuja moja kwa moja kwa ajili ya kushusha mafuta jambo
ambalo litasaidia kuondoa tatizo hilo Nchini.
Zanzibar24.
Comments