Kesi
inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal
Malinzi na wenzake wanne ya kutakatisha Dola za Marekani 173,335
imepangwa kuendelea kusikilizwa shahidi wa 10 wa Jamhuri, Januari 16,
2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Jana
kesi hiyo ilipangwa kuendelea kusikilizwa shahidi wa 10 wa upande wa
Jamhuri, lakini imeshindwa kuendelea baada ya shahidi huyo kuwa na
matatizo ya kifamilia.
Wakili
wa Serikali Mwandamizi, Leonard Swai, alidai mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kuendelea
na ushahidi, lakini shahidi waliyemwandaa amepata matatizo ya kifamilia.
Wakili
wa utetezi, Richard Rweyongeza, alidai kuwa Jamhuri walitakiwa kuandaa
mashahidi wawili tofauti ili mmoja anapopata tatizo au udhuru, mwingine
aendelee kutoa ushahidi.
"Mheshimiwa
tunaomba hili lisijirudie siku nyingine utetezi tunaomba mahakama
ipange siku mbili au tatu mfululizo za kusikiliza ushahidi," alidai
Rweyongeza.
Hakimu
Mashauri alisema kesi hiyo itatajwa Januari 2 na kusikilizwa kwa
mfululizo Januari 16, 17 na 21, 2019 na kuutaka upande wa Jamhuri uandae
mashahidi wa kutosha.
Mbali
na Malinzi washtakiwa wengine ni, Katibu wa zamani wa TFF, Mwesigwa
Selestine na Mhasibu Nsiande Mwanga, ambao wanakabiliwa na mashtaka 28
ya utakatishaji fedha.
Wengine
ni Meneja, Miriam Zayumba na Karani Flora Rauya, wote wa TFF,
wanakabiliwa na mashtaka 30 yakiwamo ya kula njama na kughushi.
Katika
kesi ya msingi ilidaiwa kuwa Malinzi, Mwesigwa na Nsiande walitakatisha
Dola za Marekani 173,335 na wako mahabusu kwa sababu mashtaka yao
hayana dhamana kisheria.
Mpekuzi.
Comments