Watendaji mahakama wafunzwa athari za rushwa.

MRAJISI wa mahakama kuu Zanzibar, Mohamed Ali Mohamed, amewataka watendaji wa idara hiyo kuisoma na kuitekeleza sheria ya utumishi wa umma pamoja na kanuni zake.
Kauli hio aliitoa wakati akifungua mafunzo kwa madereva na wahudumu wa mahakama juu ya masuala ya rushwa na utendaji wa mahakama, yaliyofanyika ukumbi wa malaria Mwanakwerekwe.
Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwapatia uelewa wafanyakazi hao ili kujua taratibu za utumishi wa umma.
Alisema mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza weledi na ufanisi katika kazi ili lengo la kuajiriwa kwao liweze kufikiwa.
Aliwashukuru washiriki kwa kukubali kujifunza mambo mbali mbali yanayohusu rushwa kwa sababu ndio adui mkubwa wa haki.
Mwenyekiti Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Assaa Rashid, alisema hakimu anatakiwa kuwa muadilifu wakati wa usikilizaji kesi na kuhakikisha kila upande unapata haki sawa.
Mmoja ya washiriki wa mafunzo hayo, Hafidh Malik, alisema mafunzo yatawasaidia kuimarisha uwezo wao wa kutoa huduma bora kwa wananchi.
Zanzibar.

Comments