Akizungumza na Zanzibar Leo, alisema kuna baadhi ya wananchi hasa
wagonjwa wa sukari wanatumia dawa za miti shamba hali ambayo
inasababisha ugonjwa huo kuwa sugu.
Alisema dawa zisizo na kiwango pia zinasababisha ongezeko la maradhi ambayo pia tiba yake kuipata inakuwa ni ya shida.
Alisema wagonjwa wengi wa sukari wanapata matatizo kutokana na
kutumia dawa za miti shamba ambazo hazijathibitishwa na wataalamu wa
afya.
Hivyo aliwaomba kuacha tabia ya kutumia dawa za asili na pale
wanapobidi basi watumie dawa zilizothibitishwa na wataalamu wa afya.
Alisema wizara itaendelea kutoa elimu ya afya kupitia vyombo vya
habari kuhusu maradhi yasiyoambukiza ikiwemo kisukari pamoja na athari
za matumizi ya dawa asili zisizothibitishwa.
Zanzibarleo.
Comments