Gazeti la Washington Post limenukuu barua ya viongozi hao wa serikali ya rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama wakimtaka rais wa sasa Donald Trump kutangaza usitishaji vita wa haraka na kukata misaada kwa askari wa muungano vamizi wa Saudia nchini Yemen.
Katika barua hiyo yumo pia Susan Rice, mshauri wa usalama wa taifa wa zamani, John Brennan, mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA, Wendy Sherman, naibu waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Marekani na Lisa Monaco, afisa wa zamani wa ngazi ya juu katika IKulu ya White House.
Aidha barua hiyo imeeleza kwamba mwaka 2015 serikali ya Barack Obama ilichukua uamuzi usio sahihi wa kuunga mkono muungano vamizi wa Saudia katika kuishambulia kijeshi Yemen na kwamba hadi sasa hakuna matumaini kwa ajili ya kuhitimishwa uingiliaji kijeshi huo wa Marekani katika vita hivyo haribifu.
Saudi Arabia kwa ushirikiano kamili wa Marekani, Israel, Imarati na baadhi ya nchi ilianzisha mashambulizi makali mwezi Machi 2015 nchini Yemen sambamba na kuizingira nchi hiyo kuanzia nchi kavu, angani na baharini.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni na asasi moja ya kimataifa ya barani Ulaya, hadi sasa zaidi ya watu elfu 80 wamekwishauawa, huku takwimu za Umoja wa Mataifa zikionyesha kwamba idadi ya wahanga wa hujuma hizo ni zaidi ya watu elfu 14.
parstoday.
Comments