Mitihani yafanyika chini ya ulinzi mkali.


MITIHANI ya taifa ya kidato cha nne iliyoanza jana, imefanyika katika mazingira ya utulivu katika baadhi ya vituo hapa Zanzibar.
Katika baadhi ya vituo kama Chuini, Nyerere, Mtopepo, Haile Sellasie, Lumumba, Vikokotoni, Kiponda, Jang’ombe  Kidongochekundu, na hata kwa upande Pemba imebainika wanafunzi wakifanya mitihani yao bila bugdha huku ulinzi ukiwa umeimarishwa.
Baadhi ya wasimamizi wa vituo hivyo, ambao hawakutaja majina yao kutajwa, wamesema mitihani inaendelea vizuri na hakuna matukio mabaya yaliyoripotiwa.
Wameipongeza serikali kwa kuimarisha ulinzi ili kuhakikisha hakuna matukio yoyote ya udanganyifu yanayotokea.
Walisema mitinani inafanyika kwa utulivu mkubwa huku wasimamizi wakitekeleza kwa vitendo kanuni zote za mitihani hiyo.
Aidha ulinzi umeimarishwa katika vituo vya mitihani ikihusisha polisi pamoja na vyombo vyengine vya ulinzi na usalama nchini.
Kwa siku ya jana watahiniwa walifanya mitihani ya Kiswahili wakati wa asubuhi na kumaliza na mtihani wa somo la uraia wakati wa jioni.
Watahiniwa laki 427,181 wamesajiliwa kufanya mtihani hiyo ambapo kati yao watahiniwa wa skuli za serekali  ni laki 368,227 na wa kujitegemea ni 58,954.

Comments