Upande
wa Jamhuri katika rufaa ya dhamana ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko umepinga rufaa hiyo na
kutoa sababu za kufanya hivyo.
Jamhuri imeweka pingamizi la awali ikiwasilisha hoja tatu za kutaka rufaa hiyo itupiliwe mbali bila hata kusikiliza msingi wake.
Katika hoja ya kwanza, Wakili wa Serikali Mkuu, Dk Zainabu Mango amesema kuwa taarifa ya kusudi la kukata rufaa si sahihi.
Amesema
kifungu cha sheria kilichotumika katika taarifa ya kusudio la kukata
rufaa hakiipi Mahakama mamlaka ya kusikiliza rufaa hiyo kwa sababu siyo
sahihi, hivyo inapaswa kutupiliwa mbali.
Katiika
hoja ya pili, Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amesema rufaa hiyo
haijakidhi matakwa ya kisheria kifungu cha 362 (1) kuhusu mwenendo wa
shauri kuambatanishwa katika rufaa.
Amesema
mwenendo wa mambo mengi yaliyotokea siku za nyuma tangu kesi ya msingi
ilipofunguliwa ambazo Mahakama ingezipata zingesaidia kuiongoza vyema
Mahakama kutenda haki.
Amesema
masharti ya dhamana ambayo kwa mujibu wa kifungu hicho yanaweza
kukatiwa rufaa lakini tangu yalipotolewa kati ya Machi na Aprili mwaka
huu hayajawahi kukatiwa rufaa, kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata
rufaa wala kuomba kuongezewa muda wa kukata rufaa.
Wakili
Nchimbi amesema kwa hali hiyo inaonyesha kuwa wakata rufaa waliridhika
na masharti hayo na hivyo haiwezekani kuja kuyaibua leo.
Baada
ya hoja hizo, Mahakama kuu imesema Kesho November 30, 2018 itatoa
uamuzi kama itatengua uamuzi wa Mahakama ya Kisutu ama kukubali .
Mbowe
ambaye ni Mbunge wa Hai na Matiko wamekata rufaa Mahakama Kuu kupinga
uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana katika kesi
ya jinai inayowakabili mahakamani hapo.
Mpekuzi.
Comments