Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba kuna makampuni 13 yamejitokeza kutaka kununua korosho kwa bei elekezi ya serikali.
Majaliwa ametoa kauli hii leo Jumatatu November 12 wakati wa zoezi la kuwaapisha mawaziri wapya walioteuliwa na Rais Magufuli.
Amesema, makampuni matano yalipeleka barua ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam huku makampuni 8 yakipeleka Dodoma.
Waziri
Mkuu ameyataja makampuni hayo kuwa ni Mega movers ambayo inataka tani
laki 2, kampuni ya Kitanzania Mkeme Agri inataka tani elfu 5, na
makampuni matatu yatachukua tani elfu 5, makampuni manne, tani elfu moja
moja.
Mpekuzi.
Comments