Baba mzazi wa mtoto huyo, Juma Khamis, alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo ambapo binti yake aliyefahamika kwa jina la Asfar Juma
Khamis, alifariki baada ya kupigwa teke la tumbo na mwenzake.
Mazishi ya mtoto huyo, yalifanyika Mahonda wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Alisema, tukio hilo lilitokea Jumamosi ambapo binti yake alirudi
kutoka chuoni na kusema anaumwa homa na kulala hadi siku ya pili.
“Siku hiyo binti yangu hakushinda vizuri, ndipo tulipopata taarifa
kwamba alipigana na mwenzake, usiku wa Jumatatu mwanangu alitapika sana
usiku ndipo asubuhi tulimpeleka hospitali,” alisema.
Alisema hospitalini alilazwa kwa ajili ya matibabu zaidi lakini kwa bahati mbaya alifariki wakati akiendelea na matibabu.
Naye Waziri Castico wakati akiifariji familia hiyo, aliwaomba wazazi
na walimu kuwafundisha watoto kucheza michezo mizuri isiyohatarisha
maisha yao.
Aidha Castico aliitembelea familia ya mwanamke aliyefariki baada ya
kupigwa rungu la kichwa na kusisitiza suala la upendo kwa familia.
Pia alipata nafasi kutembelea ofisi za Zan Tour kwa ajili ya kufuatilia masuala ya wafanyakazi na mazingira ya kazi kwa ujumla.
Zanzibarleo.
Comments