Meja Jenerali Eitan Dengut amenukuliwa na mtandao wa habari wa Ra'i al-Yawm akisema kuwa, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon inahesabiwa kuwa tishio kubwa kabisa kwa usalama wa Israe.
Jenerali huyo wa zamani wa jeshi la utawala haramuu wa Israel amebainisha kuwa, uwezo wa makombora wa Hizbullah ya Lebanaon ni hatari kwa utawala huo.
Kwa upande wake Moshe Dayan aliyewahi kuwa Naibu Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Israel ameashiria ufahamu kamili aliona Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuuu wa Hizbullah kuhusiana na hali ya ndani ya Israel amesema kuwa, hii leo Hizbullah ina makombora ya nchi kavu kwa baharini ambapo kutum ia kwake makombora hayo kkunaweza kulenga medani za gesi za utawala wa Kizayuni.
Wakati huo huo, Naftali Granot Naibu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Israel (MOSSAD) amesema kuwa, hivi karibuni Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imefanikiwa kupata teknolojia mpya ya mfumo wa kurushia makombora ambao unaongozwa kwa makini na GPS ambapo sasa inaweza kubadilisha maroketi mazito ya muqawama na kuyafanya kuwa makombora yenye umakini wa hali ya juu.
Hii si mara ya kwanza kwa viongozi na makamanda wa sasa na wa zamani wa jeshi la Israel kuonyesha wasiwasi wao mkubwa kuhusiana na uwezo wa makombora ya Hizbullah ya Lebanon.
parstoday.
Comments