Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala huo, Dk. Hussein Shaaban, zoezi hilo linaendea chini ya sheria namba 3 ya 2018.
Taarifa hiyo imefafanua kwamba zoezi hilo lilianza katika Mkoa wa Kusini Unguja siku ya Septemba 9 na linaendelea katika wilaya ya mjini tokea Septemba 29.
Alisema zoezi linahusu kuimarisha taarifa kwa wote wenye vitambulisho vya uzanzibari mkaazi pamoja na waombaji wapya na wanaobadilisha shehia.
Akitoa ufafanuzi kuhusu zoezi hilo, alisema waombaji wapya watahitaji kuwa na vielelezo vya ukaazi kutoka kwenye shehia yao mpya pamoja na vyeti vyao vya kuzaliwa.
Kwa upande wa wanaobadilisha shehia, alisema wanapaswa kuwa na vielelezo vya kutibitsha ukaazi wao kutoka kwenye shehia yao mpya.
Alisisitiza kuwa kwa mwananchi kuwa na kitambulisho na kuimarisha taarifa zake ni wajibu wa kisheria hivyo wote wanatakiwa kushiriki zoezi hilo.
Zanzibarleo.
Comments