Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewakamata aliyekuwa
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Acacia, Deo Mwanyika na
Mshauri wa Serikali ndani ya kampuni hiyo, Alex Lugendo.
Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo alisema
wanawashikilia watu hao tangu juzi, na kwamba leo wanaweza kufikisha
mahakamani kufunguiwa mashtaka kwa tuhuma zinazowakabili.
“Mwanyika
na Alex tuliwakamata kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi katika
nyanja ya madini. Wakiwa viongozi waandamizi walishindwa kusimamia nchi
ipate mapato kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa sheria.
Deo
Mwanyika alijiunga na Acacia mwaka 2001 akiwa ameitumikia kwa miaka 17,
alitangazwa kujiuzulu Agosti 24 kwa barua ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Acacia, Peter Galeta kwenda kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo.
Mpekuzi.
Comments