Uchunguzi: Mlipuko wa Ebola magharibi mwa Afrika umesababisha hasara ya dola bilioni 53.

Uchunguzi: Mlipuko wa Ebola magharibi mwa Afrika umesababisha hasara ya dola bilioni 53Virusi vya Ebola vilivyozikumba nchi za magharibi mwa Afrika hususan Sierra Leone, Guinea and Liberia mwaka 2014 vilisababisha hasara inayokadiriwa kufikia dola bilioni 53.

hayo ymekuja katika ttafiti wa Journal of Infectious Diseases ulifanyika ili kubaini mzigo wa moja kwa moja wa kiuchumi na taathira mbaya zisizo za moja kwa moja za kijamii za mlipuko wa ugonjwa huo uliokuwa mbaya zaidi duniani.
Mlipuko wa virusi vya Ebola katika eneo hilo la magharibi mwa Afrika ulioanza mwaka 2013 hadi 2016 uliua watu wasiopungua elfu 11 na mia tatu. Virusi hivyo viliziathiri zaidi nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.      
Watayarishaji wa utafiti huo, Caroline Huber, Lyn Finelli na Warren Stevens wanasema mlipuko wa Ebola huko magharibi mwa Afrika ulikuwa na taathira kubwa zaidi kwa maisha ya wanadamu.
Ugonjwa wa SARS ulioyakumba baadhi ya maeneo ya dunia mwaka 2003 ulisababisha hasara ya dola bilioni 40 na virusi vya Zika vilivyozikumba nchi za America vinakadiriwa kusabisha hasara ya dola bilioni 20.

parstoday.

Comments