Naibu waziri wa afya Zanzibar Mh. Harusi Said Suleiman
amesema serekali itaendelea kutekeleza wajibu wake katika kuwafikishia wananchi
huduma muhimu kwa kuzingatia mahitaji yanayo hitajika.
Akizungumza na watendaji wa hospitali ya chake chake mara
baada ya kuzindua vitengo vitatu ndani ya hospitali hiyo amesema muda umefika
sasa kwa wananchi wa Kisiwa cha Pemba na maeneo mengine kuzienzi huduma zinazo
tolewa ili kuweza kufikia malengo yalio kusudiwa.
Akizindua kitengo cha viuongo badia Hospitalini hapo Mh.
Harusi amesema kitaweza kuondoa changamoto za muda mrefu kwa wananchi wa Pemba
ambao walikua wakihitaji huduma hiyo kwa muda mrefu na sasa Serekali kwa
kushirikiana na wadau wa maendeleo wameweza kulitatua kwa haraka.
Amesema kitengo hicho kitaweza kuondoa changamoto ambazo kwa
kipindi kirefu wananchi walikua wakikilalamikia nakupunguza ghara kubwa ya
kuweza kuitafuta huduma hiyo kwa masafa marefu hivyo nivyema kwa wananchi
kuitumia fursa hiyo ili waweze kujikimu katika mahitaji yao kwa muda muafaka.
Amefahamisha kuwa ili kuweza kufikia malengo yaliokusudiwa
nivyema kwa madaktari kuvitumia vifaa vilivyo tolewa na kuvithamini pamoja na
kuvifanyia matengenezo pale panapo stahiki kwalengo la kuweza kuwahudumia
wananchi muda mrefu pasipo kuchakaa haraka.
Wakati huwo huwo amepata fursa ya kufungua kituo cha mkono
kwa mkono katika hospitali hiyo nakusema kuwa lengo nikupambana na matukio yote
ya udhalilishaji yasizidi kuendelea huku akiwataka watedaji wake kutoa
mashirikiano kwa walengwa.
Hatahivyo ameyashukuru
mashirika ya save the chidren pamoja na Infant Club Foot Appeal kwa kuweza
kuisaidia hospitali hiyo ambayo nikimbilio la wananchi wengi kisiwani Pemba.
Akitoa neno la shukurani kwa wafadhili walio jitokeza
kusaidia vifaa hivyo Afisa madhamini Wizara ya Afya Shadia Shaaban Seif amesema vimekuja muda muafaka kwani wataweza
kuwahudumia wananchi wanao hitaji kupatiwa msaada wa hali hiyo.
Kwaupande wake
mwakilishi wa shirika la Infant Club Foot Appeal lenye makao yake makuu nchini
Uiengereza Dr. Shault Houcking amesema wataendelea kuisaidia Zanzibar ili iweze
kufikia maendeleo endelevu kwani kila mmoja anawajibu wakufanya hivyo kwa
nafasi zao tofauti.
Nae mtaalamu wa viungo badia Dr. Salim Seif Ali amesema
wamefarajika kupatiwa vifaa hivyo ambavyo vitaweza kuwasaidia kuweza kutoa
huduma zilizobora kwa wananchi pindi wanapo hitaji.
Jumla ya vitengo vitatu vimezinduliwa katika Hospitali ya
Chake Chake ikiwa nipamoja na kitengo cha viungo bandi, Kituo cha Mkono kwa
mkono na kitengo cha Tv ambacho kitawasaidia wananchi kupata elimu ya afya na
mambo mengine.
![]() |
Mwakilishi wa ICA Dr. Shault Houcking akitoa maelezo kuhusu misaada yao.
|
Comments