SMIDA: wajasiriamali wadogo wanahitaji elimu.

Related imageMwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Wakala wa   kukuza maendeleo ya viwanda  vidogo vidogo na vya kati (SMIDA )Mussa Ame Silima Zanzibar kuna wajasiriamali wengi wenye  uoni na uelewa wa kunzisha miradi midogo midogo hivyo  kilichobaki kwa watu hao ni kupewa taaluma na mitaji ya kuwaendeleza zaidi.

Ameyasema hayo  huko katika  katika ziara ya kuwatenbea  wajasiriamali na wafanyabiashara wadogowadogo  wa mkoa wa Kusini Pemba  kuona  juhudi  na changamoto zao na kuangalia njia ya kuwasaidia kupitia mikakati na malengo ya SMIDA.

Mwenyekiti huyo amesema sio jambo rahisi kuweza kuwasaidia wajasiri amali mmoja mmoja bali SMIDA itakaa na kufanya uchambuzi kwa ajili ya  kuwaendeleza  kielimu na kujaribu kuwatafutia mikopo  itakayosaida  maendeleo ya shughuli zao .

Aidha mkurugenzi mkuu wa SMIDA Abdulhamid Idrissa Haji amesema katika mikakati yao wataanza kuwawezesha  wale walianza vizuri kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora kwa kuwatafutia soko na kuerekebisha baadhi ya miundombinu yao iliyoharibika .

Nao  baadhi ya wajasiriamali hao wameiomba SMIDA kuwapatia wataalamu vitendea kazi na safari za mafunzo ili kupata uelewa zaidi wa uzalishaji wa bidhaa bora .

Na mwandishi wetu.

Comments