Polepole: Watu Waache Nongwa, CCM Tulihangaika Sana Kuhakikisha Mo Dewji Anapatikana Baada ya Kutekwa.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole
amezungumzia kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji (Mo) na kusema
chama chao kimehangika sana kushughulikia tukio hilo, hivyo watu waache
nongwa kwakuwa matukio ya uhalifu yanatokea duniani kote.
“Unajua
watu waache nongwa, matukio haya ya uhalifu yapo duniani kote, sisi
tumehangaika sana kama chama. Wametekwa watu Afrika Kusini hili si jambo
la mzaha, watu wanatekwa kweli, kwa mfano Uingereza wametekwa watu
miaka nane hawajarudi na polisi wanasema wanafamilia wasizungumzie hii
kuonyeshwa kwamba huyo mtu hajarudi,” alisema Polepole.
Alisema kwa Tanzania kumetokea matukio mbalimbali yakiwemo ya mauaji ya watu katika wilaya za Kibiti na Mkuranga.
“Hapa
kwetu tumepata shida mara kadhaa Mkuranga na Kibiti, hili jambo sisi
ambao tupo katika uongozi wa chama na Serikali tunaona mzigo mzito,
bahati mbaya wenzetu wanafanya mzaha kwenye mambo haya makubwa,” alisema
Polepole.
Alisema
kazi ya vyombo vya ulinzi na usalama ni kuhakikisha ulinzi unaimarika,
hivyo inapotoea mtu ametekwa wao ndio wana kazi ya kufuatilia na
kuchimbua kitaalamu kwa kushirikiana na wenzao wa kimataifa.
Polepole
alisema Watanzania wamepiga maombi na dua kuhakikisha Mungu anawezesha
kila chombo kinachofanya kazi kihakikishe Mo anarudi akiwa salama na
kabariki ikafanikiwa, lakini cha kushangaza wapo watu wanaodai kuwa
mfanyabiashara huyo hakutekwa.
“Mo
amerudi anatokea mpuuzi anasema haaa, haaa Mo hakutekwa, mbona
hawakumkata vidole. Sasa wakati tunaomba Mungu mlikuwa mnategemea nini?
Unasema basi ndiyo kiongozi huyo amechaguliwa na watu.
“Baadhi
ya watu hao walioomba kuingia CCM wasahau tu, hatutachukua watu ambao
wanashindwa kuwa na utaratibu, wanashindwa kuelewa wanatamani watu
wengine wapate tabu ili waamini kweli ilikuwa tabu,” alisema Polepole.
Alisema
kitendo cha Mo kurudi bila kupata madhara yoyote ni cha kumshukuru
Mungu, na Serikali ya CCM wamevielekeza vyombo vya ulinzi na usalama
kufanya kazi mchana na usiku kuhakikisha wote wanaofanya vitendo hivyo
wanapatikana.
“Wakipatikana
washughulikiwe ipasavyo na kufanywa vitendo vyote vibaya kwa mujibu wa
sheria ili iwe fundisho kwa wengine wote ambao wanataka kufanya mchezo
na spidi kubwa ya maend.
Mpekuzi.
Comments