Naibu Waziri ataka watakatishaji fedha wafukuzwe kazi.

MAWAKALA wanaotowa huduma katika Benki ya NMB, wametakiwa kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yao, pamoja na kufanya kazi kwa uwadilifu, ili kudumisha ajira zao na kuipa hadhi benki hiyo.
Wito hu,o umetolewa na Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Hassan Hafidh, katika ufunguzi wa mafunzo ya Uwakala wa huduma za Benki ya NMB, yaliofanyika katika ukumbi wa ZSSF Kariakoo.
Jumla ya Mawakala 67 kutoka maeneo mbali mbali ya Unguja, walishiriki katika mafunzo hayo, yenye lengo la kuhakikisha kunakuwepo utoaji  wa huduma bora na kwa haraka kwa wateja wa benki hiyo  popote walipo nchini.
Naibu Waziri huyo alisema mawakala hao wana jukumu la kutowa huduma bora kwa wateja, ili kuvutiya wateja wapya, kuipa hadhi benki  ya NMB pamoja na  wao binafsi kujipatia sifa za kiutendaji.
Nae, Meneja wa NMB Zanzibar Abdalla Duchi, alisema miongoni mwa mambo yanayozingatiwa katika utoaji huduma bora za kibenki kupitia mawakala, ni pamoja na suala la usalama kwa kuhakikisha kunakuwepo usalama wa kutosha katika eneo la kutoa huduma.
Zanzibarleo.

Comments