Federica Mogherini ameyasema hayo kupitia taarifa maalumu aliyotoa kwa mnasaba wa Siku ya Umoja wa Mataifa na kubainisha kwamba, maafikiano ya nyuklia ya Iran ni moja ya mafanikio ya diplomasia ya pande kadhaa na kwamba Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa zitaendelea kuyalinda makubaliano hayo.
Katika sehemu nyingine ya taarifa yake hiyo iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya Umoja wa Ulaya, Mogherini ameongeza kuwa, zikiwa ziko bega kwa bega, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa zimekuwa na zitaendelea kuwa watetezi imara zaidi wa ushirikiano na mazungumzo.
Mkuu wa Sera za Nje wa EU amesisitiza kwamba, ni kwa sababu hiyo Umoja wa Ulaya utaendelea kutetea diplomasia ya pande kadhaa pamoja na mafanikio yake, kuanzia makubaliano ya nyuklia ya Iran ya JCPOA mpaka maafikiano ya tabianchi ya Paris na pia harakati zenye ulazima zinazofanywa na taasisi za Umoja wa Mataifa.
Hivi karibuni pia wakati alipofanyiwa mahojiano na kanali ya televisheni ya CNN, Federica Mogherini alisisitiza kuwa, Marekani haiwezi kuzitwisha maamuzi yake ya kisiasa taasisi za kimataifa na nchi zenye haki na mamlaka ya kujitawala na akabainisha kwamba, Umoja wa Ulaya utashirikiana na pande zingine kuyalinda makubaliano ya nyuklia ya JCPOA..
parstoday.
Comments