Micheweni kunufaiika na huduma za ATM.

Image result for atmKUANZA kwa ujenzi wa ATM katika Wilaya ya Micheweni Pemba, kutaondosha usumbufu kwa Wananchi kufuata huduma za Kibenki kutoka Chake Chake na Wete.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Salama Mbarouk Khatib, ameitoa kauli hiyo  wakati alipokuwa akikagua sehemu ambazo zimeanza kujegwa katika maeneo ya Micheweni mjini na maeneo ya Konde kwa hatua ya mwanzo.
Salama, alisema wananchi wa Wilaya hiyo, walikuwa wakipata tabu ya kutafuta huduma hiyo sehemu ya mbali na wakati mwengine wanapokwenda hukosa huduma hiyo, na kupata usumbufu wa kufika majumbani
mwao.

Fundi Mkuu wa kujenga ATM hizo,  Mbaraka Abdalla
Fakih, alisema ujenzi huo baada ya mwenzi mmoja utakuwa umekamilika kwa hatua ya kwanza.

Comments