Naibu huyo alieleza hayo alipokuwa akizindua kampeni maalum juu ya usalama barabarani na udhibiti wa ajali Zanzibar iliyofanyika katika viwanja vya skuli ya Jang’ombe.
Alisema, madereva na makonda wa daladala wamekuwa wakiwanyanyasa wanafunzi kwa sababu tu wanalipa nauli ndogo ukilinganisha na watu wazima.
Aidha aliipongeza taasisi ya New Vision Consortium Trainers (NVCT), kwa jinsi ilivyojitolea kutoa elimu katika maskuli juu ya kampeni za usalama barabarani.
Kwa hivi sasa wakati umefika kwa Zanzibar chini ya utaratibu ambao umenzishwa na NVCT na mimi niwahakikishie nitatumia uwezo wangu wote kuhamasisha wadau mbalimbali ili waweze kuja kuwasaidia katika kuhakikisha elimu ya barabarani inatolewa hasa kwa wanafunzi wetu katika maskuli, alisema.
Alieleza kuwa, baada ya uzinduzi huo, zitaandaliwa programu mbalimbali zikiwemo nyimbo, mashairi, michezo ya kuigiza, semina pamoja na mijadala mbalimbali katika skuli ili kufikisha ujumbe juu ya usalama barabarani.
Katika hatua nyengine Naibu huyo amewataka wamiliki wa wamiliki wa skuli wafuate sheria kwa kuacha kutumia mabasi mabovu na kujaza wanafunzi kupita kiasi na kwamba atatumia kikosi cha usalama barabarani kuhakikisha wanafunzi wanakua salama muda wote.
Alikitaka kikosi cha Usalama barabari kuwashughulikia madereva wazembe ambao wanasababisha ajali za barabarani.
Naye Mkurugenzi NVCT, Pily Khamis Layda, alisema kampeni hiyo itakuwa endelevu katika skuli zote za Unguja na Pemba na kwa sasa wameanza na skuli 10 za mkoa wa Mjini Unguja.
Aliwapongeza mabalozi wa usalama barabarani kwa jitihada kubwa wanazozichukua kupambana na usalama barabarani. Kampeni hiyo ya bila ajali ina kauli mbiu inayosema, ‘Mimi nakataa ajali wewe je?’.
Zanzibarleo.
Comments