
Nasaha
hizo zimetolewa na Shk Khalfan bin Suleiman Khalfan wakati akifungua msikiti
uliopo mkungu malofa chake chake kwaniamba ya Mufti mkuu wa Zanzibar Shkh Saleh
Qabi.
Amesema
vitendo vya baadhi ya waumini kuwashajiishisha wengine kupinga madhehebu yaw
engine nijambo linalo kinzana na maamrisho ya Allah (Sw).
Aidha
amesema nimuda sasa kwa waislam kuwakitu kimoja ili kuweza kuzitekeleza ibada
zote kwa ukamilifu pasipo namalumbano.
Hatahivyo
amewataka wafanya biashara kuiga juhudu zilizochukuliwa katika kufanikisha
mskiti huwo hadi kukamilika kwake ili iweze kutoa nguvu kwa waumini kuweza kuzitekeleza
ibada katika mazingira yaliobora.
Akitoa
neno la shukurani kwa wafadhili walio jenga mskiti huwo Shkh Zahor Saleh Omar
amesema nijambo lafaraja kuwekeza kwa Allah (SW) kwani malipo yake hayaishii
duniyani pekee nahata akhera pia malipo yake atayakuta yoyote atakae fanya
jambo jema.
Amesema
miskiti ni nyumba za Mwenyezimungu hivyo tunatakiwa kuilinda kwa halizote ili
kuweza kuinusuru dini ya Allah (SW) dhidi ya maadui wasio ipendelea mema
uislam.
Zaidi
ya milioni 300 zimetumika katika ujenzi wa msikiti huwo hadi kukamilika kwake
ambao umejengwa kwa ufadhili wa Shkh Ahmed Nassor .
Comments