Alisema hayo, kufuatia tukio la watu
kusambaza katika mitandao ya kijamii picha za utupu za mwanafunzi wa
kike, jambo ambalo ni udhalilishaji mkubwa wa kijinsia.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake Mwanakwerekwe, alisema, sheria lazima ifuate mkondo wake
kwa watuhumiwa waliosambaza picha hizo katika mitandao ili iwe fundisho
kwa wengine.
Aidha alisema tabia ya watu kusambaza
mambo mabaya katika mitandao ya kijamii inaonekana kuendelea jambo
ambalo halileti taswira nzuri katika vita dhidi ya udhalilishaji.
“Kuna mambo mengi ya maendeleo
yanayofanywa na serikali, lakini jamii haiyatangazi, badala yake
hutangaza mambo ambayo hayaleti picha nzuri katika jamii,” alisema.
“Unapomdhalilisha mtoto wakike basi
unamdhalilisha kiongozi wa baadae, unamdhalilisha mke wa mtu na pia
unamdhalilisha mama wa baadae” alifahamisha.
Alisema, mitandao ya kijamii imekuwa
jaribio la kufanyiwa ukatili watoto hali ambayo inarudisha nyuma
maendeleo ya watoto na kuathiri vizazi.
Aidha, alifahamisha kuwa, wizara watafuatilia suala hilo na kujua nani aliyesambaza picha hizo ili achukuliwe hatua za kisheria.
Sambamba na hilo, pia alisema, wiki ya
mtoto wa kike duniani kilele chake kitakuwa Oktoba 11 ambapo na kauli
mbiu kwa mwaka huu inasema ‘tumpe ujuzi mtoto wa kike kwa maendeleo
endelevu’.
Aliwaomba wananchi kuacha muhali katika
vita dhifi ya udhalilishaji na badala yake wawafichue watu wanaotenda
vitendo hivyo hata kama ni jamaa zao.
Zanzibarleo.
Comments