Alisema mikakati mbali mbali tayari imewekwa katika mpango kazi wao, kupitia Mradi wa SWIOFISH ambao unatekelezwa Zanzibar, ili kuona wakulima wa mwani wanaoinuka kimaisha kupitia kilimo chao hicho.
Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa Msafara wa wajumbe wa Benk ya Dunia nchini Tanzania, Damiel Mira Salam, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara ya kuangalia miradi inayotekelezwa na benki hiyo Kisiwani Pemba,
Alisema bado ukulima wa Mwani unakabiliwa na changamoto, mbali mbali ikiwemo ya uanikaji wake hasa kipindi cha mvua, ulimaji wake hauko vizuri pamoja na wakulima wenyewe kukosa vitu muhimu vinavyoweza kuwafanya wakalima bila ya hofu.
Mkuu huyo wa msafara alisema kutokana na hali hiyo, watahakikisha wanashirikiana na Wizara husika, ili kuona namna wakulima wa Mwani hasa wanawake wanaweza kuboresha kilimo chao hicho kwa muda mrefu.
Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya uvuvi Zanzibar, Mussa Aboud Jumbe, alisema mradi huo ni wa kipindi cha miaka sita na sasa umeingia katika miaka mitatu ya mwisho, ambapo wadau hao wamaendeleo wamekubali kuingiza masuala ya miradi ya mwani.
Zanzibarleo.
Comments