Alisema hayo wakati akizungumza na
wazazi, walimu na wananchi wa Maziwang’ombe, baada ya kuweka jiwe la
msingi skuli ya maandalizi Maziwang’ombe.
Alisema elimu ndio kitu muhimu katika maisha ya kila mtu, hivyo lazima watoto wa kike wapatiwe elimu badala ya kuozeswa waume.
“Hipendezi sisi wazazi kuwaozesha watoto wetu badala yake tuwaachie wasome, kwa ajili ya maisha yao ya baadae,” alisema.
Aidha aliwashauri walimu kutowatoza
fedha wanafunzi, kwani serikali imejidhatiki kulipia gharama zote
zinazowahusu wanafunzi wa msingi na sekondari.
Aidha alisema serikali imedhamiria kuwapatia elimu bora watoto, kwa kuanzia na ngazi za maandalizi hadi sekondari.
Alisema kujengwa kwa skuli ya
maandalizi Maziwang’ombe, kutawahamasisha watoto kusoma kwa bidii na
serikali kufikia malengo yake.
Akizungumzia skuli Micheweni, alisema
serikali inaendelea kutoa fursa kwa wanafunzi kusoma mpaka kiwango
wanachotaka, kwani fursa za kufanya hivyo zipo.
Alikemea kitendo kilichofanywa na
baadhi ya wananchi kuzuia ujenzi wa ukuta wa chuo cha CCK Micheweni,
huku akiutaka uongozi wa chuo hicho kujenga ukuta kwani ardhi ni mali ya
serikali.
Akizungumza na walimu ambapo skuli zao
zimefanya vizuri na kupata daraja la kwanza, alisema sasa umefika wakati
wa kushindanisha mikoa ili kupasisha wanafunzi wengi wa kidato cha sita
na nne.
“Naamiamini mikoa ya Pemba inaweza
kufanya vizuri, mjini magharibi pia, hata mikoa yote itafanya vizuri,
kazi kubwa mlionayo ni kuwasomesha vijana wetu,” alisema.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali,
Riziki Pembe Juma, aliwaomba wafanyabiashara kujitokeza kusaidia sekta
ya elimu, kama anavyofanya mfanyabiashara Said Nassir Nasoor (Bopar).
Zanzibarleo.
Comments