Abiria wote 188 wafa ndege ikianguka Indonesia.

Ndege mpya aina ya Boeing 737 MAX 8 ya shirika la Lion Air iliyokuwa imebeba abiria 188 ikielekea mji wa Pangkal Pinang, ilianguka baharini Jumatatu muda mfupi baada ya kupaa kutoka Jakarta, maofisa wa Indonesia walisema.
Ndege hiyo iliyopangiwa safari nambari JT-610 ilikuwa inakwenda Pangkal Pinang, jiji linalopatikana katika visiwa vya Bangka Belitung. IIitoweka kutoka kwenye mitambo ya rada saa kadha baada ya kupaa, ilipokuwa inavuka bahari.
Katika kikao na wanahabari, maofisa walisema ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 178 watu wazima, watoto watatu, marubani wawili na wahudumu watano.
Msemaji wa shirika la uokoaji na kutafuta manusuera, Yusuf Latif aliwaambia wanahabari: "Imethibitishwa kwamba ndege hiyo imeanguka."

Comments