
Mhe. Waziri amezungumza hayo jana katika halfa ya utoaji wa zawadi kwa wanafunzi walio maliza kidato cha sita ambao wamefanikiwa kufauli kwa kiwango cha daraja la kwanza kwa mwaka 2018, katika ukumbi wa hoteli ya Misali Mkoa wa kusini Pemba.
Mhe. Pembe aliwasisitiza wanafunzi wa kike wasikubali kushawishika kwa chochote kile kwani lengo la kwenda chuoni ni kusoma na sivinginevyo. Hata hivyo aliwasihi waweze kujitambua na wawe wazelendo wa nchi yao na wajitahidi sana katika masomo yao ili wakimaliza warudi kuindeleza nchi yao.
Aidha, aliwataka wanafunzi wanaoendelea na masomo yao wajitahidi zaidi nao waweze kufaulu vizuri zaidi na kuwasihi waitumie nafasi vizuri kwa lengo la kuengeza ufaulu ili mwakani iwe mara mbili zaidi.
Pia aliwazawadia Komputa mpakato (laptop) wanafunzi 30 waliopata daraja la kwanza kwa skuli za Pemba na alitoa zawadi nyengine kwa jitihada zaidi ya kila mwanafunzi.
Hata hivyo aliwapongeza walimu pamoja na wazazi kwa kushirikiana kwa pamoja na kufanya kazi kubwa kwa wanafunzi hao na pia aliwasihi wazidishe juhudi zaidi ili kuweza kutoa matokeo mazuri zaidi mwakani.
Comments