vinatarajiwa kupitisha katika hatua zilizobaki miswada mitano ya sheria ikiwemo Muswada wa Sheria ya Bodi ya Kitaalama ya Walimu Nchini
wa mwaka 2018.
Pia, mkutano huo utashuhudia kiapo cha uaminifu kwa Mbunge mteule wa Buyungu (CCM) Christopher Chiza aliyechaguliwa Agosti 12, 2018.
Uchaguzi huo wa Buyungu, ulifanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Kasuku Bilago kufariki dunia Mei 26, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa iliyotolewa leo Septemba 3, 2018 na kitengo cha Habari kwa Umma na Mawasiliano cha ofisi ya Bunge imesema miswada mingine ambayo tayari ilishasomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa 11 ni Muswada wa Sheria ya Kulitangaza jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi wa mwaka 2018.
Miswada mingine ni; wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali namba 2 wa mwaka 2018 Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali namba 3 wa Mwaka 2018, Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2018.
Katika mkutano huo, Kamati ya Sheria Ndogo itawasilisha taaarifa zake bungeni zinazohusu uchambuzi wa sheria ndogo kwa ajili ya kujadiliwa na wabunge.
Taarifa hiyo imesema mkutano huo utakaomalizika Septemba 14 mwaka huu, utakuwa na wastani wa maswali 125 ya kawaida yanayotarajiwa kuulizwa na wabunge na wastani wa maswali 16 ya papo kwa papo kwa waziri mkuu.
Comments