Ujerumani imekuwa nchi ya kwanza kufungua ofi si ndogo mjini Dodoma, iliyozinduliwa mjini hapa jana.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa ofisi hiyo ya mawasiliano, ambayo itafanya pia
shughuli za kibalozi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Augustine Mahiga alisema hatua hiyo ni ishara chanya kwa nchi
nyingine kufungua ofisi zao jijini Dodoma.
“Tunajua
Umoja wa Mataifa umefungua ofisi yake ya mawasiliano hapa jijini
Dodoma, lakini kwa upande diplomasia ninyi (Ujerumani) mmekuwa wa kwanza
kufungua ofisi ndogo na huu ni mwelekeo mzuri wa kuhamia kabisa jijini
hapa na pia ni ishara chanya kwa mataifa mengine kuhamia Dodoma,”
alisema.
Mahiga
aliongeza, mara nyingi historia inajirudia, wakati leo (jana)
tunasherehekea uzinduzi wa ofisi ndogo ya ubalozi wa Ujerumani,
takribani miaka 100 iliyopita Ujerumani walikuwa wakisherehekea kufikia
nusu ya ujenzi wa Reli ya Kati.”
Alisema Ujerumani imekuwa na uhusiano wa miaka mingi na kuwa nchi ya kwanza kuiingiza Tanzania kwenye uchumi wa dunia.
Mahiga
aliiomba Ujerumani kuwa mstari wa mbele na mbia wa kuisemea Tanzania
katika mashirika ya kimataifa kama Umoja ya Ulaya (EU), na Baraza la
Umoja wa Mataifa la Ulinzi na Usalama na kuongeza kuwa ajenda zote za
nchi, zitakuwa zikijadiliwa hapa nchini.
Balozi
wa Ujerumani nchini, Dk Detlef Waechter alisema ofisi yake imefungua
ofisi ndogo ya Wakala wa Ujerumani wa Maendeleo (GIZ) na (KFW) pamoja na
Ubalozi wa Ujerumani uliopo Dar es Salaam baada ya kuwapo kwa ongezeko
la uhitaji.
“Karibu
serikai yote ya Tanzania imeshahamia katika mji mkuu, tumeona ongezeko
la uhitaji wa kutafuta njia ya kuendeleza ushirikiano katika nyanja zote
kwa kiwango kile kile, ukaribu na urafiki wetu,” alisema.
Aliongeza:
“Hii ndio sababu watendaji watatu wa Ujerumani katika nchi hii
wameungana na kusema tufanye mpango wa kufungua uwakilishi Dodoma”.
Dk
Waechter alisema Ujerumani inajua kuwa nchi kuhamisha makao yake makuu
huchukua muda mrefu na kupitia changamoto kadhaa. Alitoa mfano hatua ya
nchi yake iliyohamisha makao makuu yake kutoka mji wa Bonn kwenda
Berlin.
“Tukiwa
katika mwaka wa 30 tangu kuanza kuhamisha Makao Makuu ya nchi, asilimia
50 ya watumishi wa serikali bado wanafanya kazi zao si katika mji mkuu
mpya wa Berlin, ila bado wako Bonn.”
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge aliwahakikisha ulinzi na usalama
kwa Mkoa wa Dodoma na kuongeza kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada
za kuboresha miundombinu na huduma ili kuhakikisha watu wa mataifa yote
wanaishi wa usalama.
Mpekuzi.
Comments