Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema kuwa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndio wanachelewesha kukamilika kwa
ripoti ya uchunguzi dhidi ya shambulio la mbunge wa Singida Mashariki
Tundu Lissu.
Waziri
Masauni ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali laMbunge wa Ubungo
(CHADEMA) Saed Kubenea bungeni leo Septemba 14, ambalo lilihoji kuwa
kumekuwa na matukio mengi ya kihalifu yanatokea ikiwemo kupotea na
kutekwa watu, lakini serikali imekuwa ikionesha kuwalinda zaidi watu wao
wa karibu na sio wanaharakati wanaoipinga serikali na kuhoji ni lini
ripoti ya serikali itakamilika kuhusiana na tukio la kushambuliwa kwa
mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.
Masauni
amemtaka Kubenea kufuta kauli yake aliyodai kuwa ni upotoshaji kwa
jamii kwani hakuna matabaka katika ulinzi wa raia na mali zao na kusema
kuwa; “Napenda kujibu swali la Kubenea lakini ningependa kumpinga na
kumkosoa vikali kwa kauli yake, kwani hakuna matabaka katika kulinda na
kusimamia usalama wa raia na mali zao wote na hakuna matabaka, kuhusu
shambulio la Tundu Lissu chama chao hakitoi ushirikiano ikiwemo kumficha
dereva ambaye ndiye shuhuda namba moja”.
Aidha
Masauni ameongeza kuwa masuala ya kigaidi yanahitaji muda zaidi
kukamilisha uchunguzi wake kwakuwa huhusisha taasisi nyingine za nje
zaidi ya Jeshi la polisi hivyo unahitaji muda na umakini wa hali ya juu.
Suala
la watu wasiojulikana limekuwa likiibua mvutano bungeni kila ifikapo
zamu ya kuchangia kwa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kuibuka
kwa matukio ya utekaji na kupotea kwa watu maarufu kuanzia mwaka 2017
wakiwemo wanahabari na wasanii wa muziki.
Mpekuzi.
Comments