Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemuomba Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt Joh Pombe Magufuli kufanya ziara ya mara kwa
mara kwa Mkoa wa Dar es salaam ili kuwawezesha wananchi wa mkoa huo
kumuona kiongozi huyo.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa matumizi ya barabara ya juu Flyover Tazara jijini
Dar es salaam Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amemuomba Rais Magufuli
kuiongeza Dar es salaam kwenye ziara zake ili aweze kukutana na wananchi
wa jiji hilo.
“Mheshimiwa
Rais sina mengi ya kuomba kwako zaidi ya kukuomba unapofanya ziara zako
mkoani uwe unakuja na Dar es salaam walau uwe unakutana na wananchi wa
Mbagala, Yombo, pamoja na maeneo mengine maana hawa huwa wanakukumbuka
sana, pia huwa tunaona wivu unapofanya ziara mikoani lakini kwetu
hatukuoni.” Amesema Makonda
Aidha
mkuu wa huyo mkoa ameeleza Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni
linaingiza shilingi milioni 800 kwa mwezi kupitia tozo zinazotolewa na
watumiaji wa daraja hilo pamoja na kueleza changomoto ya
utapeliunaofanywa na baadhi ya madalali Dar es salaam kwa kushirikiana
na taasisi za kifedha.
Mpekuzi.
Comments