Jana
September 22, 2018 ndio ilikuwa harambee ya kuchangia Programu
iliyoanzishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kwa ajili ya
kutokomeza Zero.
Program
hiyo imelenga kuinua kiwango cha ufaulu wilayani humo kwa kuhakika
wanafunzi wanakuwa na madarasa mazuri ya kusomea, vifaa na chakula.
==>.Soma taarifa kamili ya Jokate Mwegelo hapo chini;
Kutokana
Na Maombolezo Ya Msiba Ukerewe, Serikali ya Wilaya ya Kisarawe kwa
pamoja tuliamua kuhairisha shamrashamra za programu yetu ya Tokomeza
Zero Harambee Pale Minaki Sekondari, tukasimama na kuombea ndugu zetu
waliopoteza maisha lakini pia kutoa faraja kwa kuchangia Milioni Moja
kama rambirambi kutoka Wilaya ya Kisarawe. .
Lakini
tuliruhusu waliofika kuchangia na baada ya kupiga mahesabu leo tumeweza
kuchangisha Milioni 125.062 katika awamu hii ya kwanza. Hii ahadi ya
michango ya pesa taslimu imevuka lengo letu la awali ambalo lililuwa ni
Milioni 100 ilituweze kuhudumia makambi ya wanafunzi mpaka mwezi wa kumi
na moja ambapo wataanza mitihani yao ya mwisho ya taifa. .
Napenda
kuchukua fursa hii kuwashukuru sana wananchi wenyeji wa Kisarawe kwa
kuitikia wito kwa wingi sana ila pia na wadau wetu kutoka nje ya
Kisarawe. Tunawashukuru sana. Mungu awaongezee pale mlipopunguza. .
Kwa
kipekee nimshukuru Ndg. Masanja Kadogosa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika
La Reli Tanzania (TRC) na Wakandarasi Yepi Merkezi kwa kuahidi kujenga
madarasa wenyewe na kuchangia chakula kwenye makambi yetu. Reli ya
Kisasa inayojengwa inapita Kisarawe na tunawezesha ujenzi huu kwa
ku-supply malighafi za ujenzi. Kwahiyo Kisarawe ni wadau wakubwa wa TRC.
.
Naendelea
kuwakaribisha wadau mbalimbali kutuunga mkono kwenye Programu hii ya
Tokomeza Zero awamu zinazofuata ni kuboresha mazingira ya kusoma na
kufundisha ikiwa ni kuhakikisha miundombinu mbalimbali ya Elimu
inapatikana. Na pia tutakuwa na Tokomeza Zero Inspirational Talks -
kufuata wanafunzi na jamii walipo na kuongea nao juu ya umuhimu wa
Elimu.
Mpekuzi.
Comments