Mgombea ubunge Chadema jimbo la Liwale huyu hapa.



Mwenyekiti wa CHADEMA, FREEMAN MBOWE Chadema kimemteua Juma Rashid Upinde kuwa mgombea ubunge jimbo la Liwale katika uchaguzi wa Oktoba 13.
Taarifa iliyotolewa leo Septemba 13, imeeleza kuwa uamuzi huo umefanywa na Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi Septemba 10, jijini Dar es Salaam.
“Kamati Kuu ya Chadema imefanya uteuzi huo kutokana na mamlaka iliyonayo kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya mwaka 2006, toleo la mwaka 2016, ibara ya 7.7.16(q),” imeeleza taarifa hiyo.
Kadhalika taarifa hiyo imesema  Upinde ni mwanachama mwandamizi wa Chadema, Kanada ya Kusini(Lindi, Mtwara na Ruvuma) na ameshiriki kukijenga na kukiimarisha chama katika maeneo hayo.
Imeeleza kuwa Upinde tayari ameshachukua fomu ya kugombea ubunge jimbo hilo na leo Septemba 13, atarejesha.
Kampeni za uchaguzi zitaanza Septemba 14 hadi Oktoba 12 mwaka huu.

Comments