Jumuiya hiyo imetangaza kuwa, boti kadhaa zilizokuwa zimebeba
wahajiri hao haramu zimeokolewa ikiwemo boti moja iliyokutwa katika maji
ya karibu na kisiwa cha Majorca.
Idadi ya wahajiri haramu wanaoelekea Ulaya imeongezeka sana nchini
Uhispania katika miezi ya hivi karibuni baada ya Italia kukataa kupokea
wahajiri hao.
Italia imesimamisha huduma zote za misaada ya kibinadamu
kwa wahajiri wanaowasili pwani ya nchi hiyo, suala ambalo linawafanya
wahajiri wengi kuelekea Uhispania.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu zaidi
ya wahajiri 300 waliokuwa mbioni kuelekea Uhispania pekee wamefariki
dunia baada ya kuzama katika Bahari ya Mediterrania.
Idadi ya wahajiri
wote waliofariki dunia mwaka huu katika Bahari ya Mediterrania
wakielekea Ulaya ni 1600.
parstoday.
Comments