Mabula awatuliza wananchi kijiji cha soga mkoa wa pwani kuhusu mgogoro wa ardhi dhidi ya muwekezaji.

Mabula alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara katika kijiji hicho kwa ajili ya kushughulikia mgogoro wa ardhi
baina ya wananchi wa kijiji hicho na kampuni ya Mohamed Enterprises
inayomiliki eneo kubwa katika kijiji hicho jambo linalowatia hofu
wananchi kuondolewa katika eneo hilo.
Aliwaambia wakazi wa kijiji hicho kuwa lengo la ziara yake ni kujionea
hali halisi ya eneo kwa kuwa ni vigumu kutatua mgogoro bila kufika
katika eneo la tukio.
Alisema, serikali imesikia kilio cha wananchi hao ambao wapo tangu mwaka 1975 na serikali haiwezi kuwafukuza kwa kuwa iko kwa ajili yao.
Kwa mujibu wa Mabula, Serikali inachoangalia sasa kama muwekezaji ameshindwa kuendeleza eneo alilomilikishwa kulingana na masharti basi umiliki utafutwa na katika ngogoro wa eneo hilo tayari Afisa Ardhi Mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijni amepeleka mapendekezo ya kufuta sehemu ya umiliki wa shamba hilo kutokana na ukiukwaji masharti ya uwekezaji.
‘’Kinachosubiriwa sasa ni mchakato mzima na suala hilo na tayari lishapelekwa kwa mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua za utekelezaji’’ alisema Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mabula alimuagiza mkuu wa Wilaya ya Kibaha Asupta Mshana kuhakikisha hakuna mwananchi yoyote anayenyanyaswa kuhusiana na mgogoro huo na kusisitiza watakaofanya hivyo basi hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Awali wananchi wa kijiji hicho walitoa malalamiko yao kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa wamekuwa wakinyanayswa na muwekezaji kwa madai ya kuvamia eneo lake wakati wao walikuwemo tangu mwaka 1975.
Mkazi wa kijiji hicho Joseph Masana alisema, wananchi wa eneo hilo hawakatai uwekezaji bali wanahitaji uwekezaji shirikishi ambapo muwekezaji atakuwa aenaendeleza mashamba badala ya kuyaweka kuwa mapori.

Comments