Kijana mlemavu wa Kipalestina afungwa jela miaka 35 na Israel.

Kijana mlemavu wa Kipalestina afungwa jela miaka 35 na IsraelMahakama moja ya utawala haramu wa Israel imemhukumu kifungo cha miaka 35 jela kijana mlemavu wa Kipalestina kwa madai ya kuwashambulia askari wawili wa utawala huo katili.

Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Wilaya ya Jerusalem (Quds) lilitoa hukumu hiyo jana Jumatano, dhidi ya kijana wa Palestina mwenye umri wa mika 21 kwa jina la Ayman Kurd.
Maafisa wa utawala wa Kizayuni wa Israel walidai kuwa, kijana huyo mlemavu ambaye hawezi kutembea na anatumia kiti cha magurudumu aliwashambulia kwa kisu askari wawili wa utawala huo wa Kizayuni mjini Quds mnamo Septemba 19, 2016 na kuwajeruhi.
Kwa mujibu wa takwimu za Kundi la Haki za Binadamu la adh-Dhamir la Palestina, takribani Wapalestina 7,000 wanashikiliwa katika magereza ya utawala haramu wa Israel huku wakiwa katika mazingira mabaya kabisa.
Inaelezwa kuwa, kati ya maelfu ya Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala wa Kizayuni wa Israel, zaidi ya 60 miongoni mwao ni wanawake na wengine 300 ni watoto.
Wazayuni wakiwa na nia ya kufikia malengo yao ya kujipanua, kila siku wamekuwa wakishambulia maeneo ya Wapalestina na kuwatia mbaroni makumi ya raia hao wasio na ulinzi.
parstoday.

Comments