Kiir na Machar watia saini makubaliano ya amani Sudan Kusini.

Kiir na Machar watia saini makubaliano ya amani Sudan KusiniRais Salva Kiir wa Sudan Kusini na hasimu wake wa kisiasa, Riek Machar jana walitia saini makubaliano ya amani katika mkutano uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Ripoti zinasema kuwa makubaliano hayo ni hatua mpya katika njia ya kuhitimisha vita vya ndani nchini Sudan Kusini vilivyoanza miaka mitano iliyopita. 
Tarehe 28 Juni pande hizo hasimu zilitia saini hati ya kusitisha vita daima mjini Khartoum katika sherehe iliyohudhuriwa na viongozi wa nchi za Sudan na Uganda na siku kadhaa baadaye walikubaliana juu ya kuondoa majeshi na wapiganaji wao katika maeneo ya mijini na makazi ya raia. 
Hata hivyo baada ya kutiwa saini makubaliano ya kusitisha vita, jeshi la serikali ya Juba na waasi wanaoongozwa na makamu wa zamani wa Rais wa Sudan Kusini, Riek Machar zilituhumiana kukiuka makubaliano hayo. 
Nchi ya Sudan Kusini ilijitenga na Sudan mwaka 2011 kwa uchochezi wa nchi za Magharibi hususan Marekani. Mwezi Disemba mwaka 2013 nchi hiyo changa zaidi duniani ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha vito vya maelfu ya watu na mamilioni wamelazimika kuwa wakimbizi.  
parstoday.

Comments