Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHEDEMA) kanda ya Kaskazini, kimelalamikia
kitendo cha mawaziri kujitokeza na kufanya kampeni za uchaguzi mdogo
jimbo la Monduli na kimeeleza kitawafikisha kwenye kamati ya maadili ya
taifa.
Katibu
wa chama hicho kanda ya Kaskazini ambaye pia ni mwenyekiti wa chama
mkoa wa Arusha, Amani Golugwa amesema mbali na malalamiko yao ya
kutotendewa haki katika uchaguzi uliofanyika jana lakini watawashtaki
mawaziri waliopiga kampeni.
''Sisi
kama viongozi tulijipanga vyema kuanzia kampeni tumeona uvunjivu wa
sheria mwingi na tumerekodi kila kitu ikiwemo mawaziri kuja kufanya
kampeni huku wakiahidi utekelezaji wa miradi kitu ambacho ni kinyume na
sheria ya uchaguzi hivyo tutawafikisha kwenye kamati ya taifa ya
maadili'', amesema.
Amani
Golugwa amewataja baadhi ya mawaziri waliofika jimboni Monduli wakati
wa kampeni na kutoa ahadi ni pamoja na waziri wa Ardhi William Lukuvi,
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso, pamoja na Naibu waziri wa Madini Mhe.
Doto Mashaka Biteko.
Aidha
Golugwa amefafanua kuwa katika kipindi hicho cha kampeni walishuhudia
mawaziri hao wakitoa ahadi na kufanya baadhi ya mambo ambayo kimsingi
yapo kinyume na sheria na taratibu za uchaguzi.
Mpekuzi.
Tufuatilie kupitia ........... https://www.youtube.com/channel/UCc_TYuIr0heTGwcQfHENDmA
Comments