Rais
Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(SUMATRA) Mhandisi Dkt. John Ndunguru na kuivunja bodi hiyo kuanzia leo Septemba 24, 2018.
Rais
Magufuli amechukua hatua hiyo kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha
MV. Nyerere iliyotokea Septemba 20, 2018 na matukio mbalimbali ya ajali
za barabarani hapa nchini yanayosababisha vifo, ulemavu na uharibifu wa
mali.
Pamoja
na hatua hiyo kamati ya uchunguzi ambayo itatangazwa na Waziri Mkuu
Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa baadaye leo, itaendelea na uchunguzi wa
ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na
usalama kama ilivyopangwa.
==>>Hapo chini ni taarifa ya IKULU
Comments