WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dk. Philipo Mipango, amezitaka benki zote nchini
kuanza kuwachunguza wafanyakazi wao na wasiowaadilifu ili wachukuliwe
hatua. Waziri Mpango amesema lengo la agizo hilo ni kuzijengea benki
imani kwa wateja wao.
Aliziagiza benki zote kufanya uhakiki na kuwachunguza wafanyakazi wao wote ili kutambua ambao sio waaminifu.
Aidha,
ameliagiza Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza
matukio ya uhalifu yanapotokea kwenye benki na kwamba endapo wafanyakazi
watabainika kupanga njama, uongozi wa benki husika uwachukulie hatua za
kisheria.
Waziri Mipango alisema hayo wakati wa ufunguzi wa tawi la Benki ya Amana jijini hapa kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Aidha,
alilitaka Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua
hatua kwa benki zitakazobainika wafanyakazi wake kuhusika katika tukio
lolote la wizi wa fedha za wateja.
Dk. Mpango pia alizungumzia matukio ya watu kuvamiwa na kuporwa baada ya kutoka kwenye benki.
Alieleza
kuwa matukio ya wateja kuporwa fedha wanapotoka benki ni ya kutisha na
kwamba yanatokana na baadhi ya wafanyakazi ambao siyowaadilifu na
waaminifu kushirikiana na wahalifu hao.
Alitaka
matukio hayo yafike mwisho kwa wafanyakazi kuchunguzwa na kwamba benki
ambayo haitafanya uchunguzi kwa wafanyakazi wake na likatokea tukio kama
hilo, viongozi wake wawajibike.
Alisema
lengo la zoezi hilo ni kujenga imani kwa wateja kwa kuwa matukio hayo
yanawafanya kuona benki siyo mahala pa siri na si salama tena kwa
usalama wao na mali zao.
Mpekuzi.
Comments